NENO LA LEO

HII NDIYO JUMLA YA MANENO YOTE YAMEKWISHA SIKIWA MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE ! HII NDIYO JUMLA YA MANENO YOTE YAMEKWISHA SIKIWA MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE

Friday, 17 March 2017



**LESONI**
  
Ijumaa ya leo 17 Machi 2017Maandalio ya Sabato ya BwanaTafakari zaidi 
 Ukweli dhahiri kuwa watu wanauliza kwa shauku endapo wametenda dhambi isiyosameheka hudhihirisha kuwa kwa hakika hawajafanya hivyo. Kama wangelikuwa wameitenda, kwa hakika wasingelihofia jambo hilo. Hofu yao ndio ushahidi hasa wanaouhitaji kwamba, kwa kweli, bado wako tayari kwa ajili ya uongozi wa Roho. Anachotakiwa kufanya mtu huyo ni kudai haki ya Yesu na, kushikilia sifa stahilifu za Yesu, kusonga mbele katika imani na utii. Ni kwa njia ya kufunikwa na haki ya Kristo pekee, ambayo ni “haki ya Mungu” (Rum. 10:3), ndipo anapoweza kupata amani na uhakikisho ambao sasa wanapungukiwa sana.Kwa kweli, kuna mtu mmoja ambaye Mungu hawezi kumsamehe, na huyo ni mtu anayeendelea kukataa kuja kwa Yesu ili aweze kupewa msamaha. “Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu haitokani na neno au tendo lolote la ghafla; lipo katika upinzani thabiti na wa makusudi dhidi ya kweli na ushahidi husika uliotolewa.”— Ellen G. White Comments, The SDA Bible Commentary, vol. 5, uk. 1093. “Hakuna mtu yeyote anayepaswa kuiangalia dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu kama kitu fulani cha siri na kisichoweza kujulikana. Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni dhambi ya kuendelea kukataa kuitikia mwaliko wa toba.”—Ellen G. White Comments, The SDA Bible Commentary, vol. 5, uk. 1093.

Nakutakia maandalizi mema ya Sabato

Tuesday, 14 March 2017

UBATIZO NA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU

(Yohana 4, Matendo 1, 1 Wakorintho 12)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye

ROHO MTAKATIFU

(Waefeso 1, 1 Wakorintho 12) Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano).